Masharti ya Majukumu ya Kamati ya Tuzo ya Tuzo la Mo Ibrahim la Kufaulu kwa Uongozi wa Kiafrika
- Halmashauri ya Wakfu wa Mo Ibrahim itateua Kamati ya Tuzo yenye watu waadilifu na wanaowajibika. Kutakuwa na uwakilishaji mpevu wa Waafrika, kukiwa na usawa wa rangi na kijinsiya pasipokuwa na kule kugongana na kazi nyingine za kibinfasi. Kamati ya Tuzo itashirikisha wanachama wawili kutoka kwa Halmashauri ya Wakfu.
- Wanachama wa kamati ya Tuzo watafanya kazi kwa kipindi cha muda wa miaka mitatu. Ingawa wanachama wanaweza kujitolea kutaka kuteuliwa kwa kipindi kingine, kunatarajiwa mabadiliko katika Kamati ya Tuzo. Watu binafsi wanaweza kuteuliwa kwa vipindi vifupi ili wengine nao wapewe nafasi.
- Wanachama wa Kamati ya Tuzo watatarajiwa kuzingatia maadili yanayoambatana na Tuzo lenyewe na wanatarajiwa kuwa huru huria, waadilifu, na wasiwe na mapendeleo yoyote. Wanachama wanaweza kungÕatuka toka uanachama wa Kamati ya Tuzo wakati wowote ule, kwa sababu zozote zile, bora atoe ilani kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ama Halmashauri ya Wakfu.
- Kamati ya Tuzo itasaidiwa na Afisi kuu ya Wakfu.
- Kamati ya Tuzo itakutana mara mbili kwa mwaka: Mara ya kwanza kuitayarisha mipango yake na mara nyingine kufanya uteuzi wa mwisho wa Mshindi. Wanachama wote wa Kamati ya Tuzo sharti wawe pale kwa vyovyote vile. Wanachama wa Kamati ya Tuzo pia watakuwa na jukumu muhimu katika kuasisi na kulitoa Tuzo la Mo Ibrahim.
- Katika mkutano wa kwanza, Kamati ya Tuzo itaidurusu orodha ya wanaopigania Tuzo la Mo Ibrahim.
- Wanaoshiriki ni viongozi wastaafu wa mataifa ama serikali za Afrika chini ya Sahara ambao wamepata uongozi kwa njia ya uchaguzi wa kidemokrasia na ambao wametoka mamlakani miaka mitatu iliyopita, na ambao wametimiza miaka ya uongozi kwa mujibu wa katiba.
- Kamati ya Tuzo itaidurusu mipango ya sasa inayoendelea ya Kigezo cha Mo Ibrahim cha Uongozi wa Kiafrika.
- Kamati ya Tuzo itaipa jukumu Afisi kuu kwa masiala ya kiutafiti, hususan kwa msingi wa kufahamu wazi ni nani anaweza kushiriki kwa mujibu wa Kigezo cha Mo Ibrahim cha Uongozi wa Kiafrika, na yumkini kuhusisha mambo mengine pia.
- Kabla ya mkutano wa pili wa Kamati ya Tuzo, Afisi Kuu, ikiongozwa na mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo, itatayarisha vifaa vya utafiti kama vinavyohitajika.Inapohitajika, hii inaweza kutolewa faraghani kwa wanachama wa Kamati ya Tuzo kwa muda tu.
- Katika mkutano wa pili, Kamati ya Tuzo itajadili na kumteua Mshindi wa Tuzo la Mo Ibrahim.
- Mkutano utakuwa wa faragha, na utaendelea hadi pale Mshindi atakapoteuliwa, ama
- Kamati ya Tuzo kuamua kwamba Mshindi hayupo mwaka huu. Maamuzi yatarekodiwa.
- Watakaohudhuria pekee ni Wanachama wa Kamati ya Tuzo na Mkurugenzi Mkuu wa Wakfu.
- Kawaida, mkutano utagawanywa katika awamu mbalimbali-
- kwanza kabisa kuchunguza matokeo ya Kigezo cha Ibrahim na taathira zake
- kudurusu wanaoshiriki(ikiwemo vitu vyovyote vya kimsingi vilivyotayarishwa na vitendo vya nchi zao wakati walipokuwa mamlakani kwa mujibu wa Kigezo na kwa upana zaidi)
- kutayarisha orodha teule ya washiriki
- kuzingatia ubora wa washiriki teule
- kumteua Mshindi( ama kuamua kuwa hakuna mshiriki yeyote anayestahili hadhi hiyo mwaka huu)
- kutoa kwa umma sababu za uamuzi-darubini ikimlenga Mshindi tu wala sio washiriki wengine.
- Kuhairisha kikao kwa minajili ya kujitayarisha kutoa taarifa kwa umma.
- Kukutana tena ili kuikubali ile taarifa rasmi ya kutolewa kwa umma.
- Halmashauri ya Wakfu itakuwa tayari kulipokea na kulikubali rasmi pendekezo la Kamati
- ya Tuzo. Afisi Kuu itatarajiwa kuwasiliana na Mshindi na/ama wafanyikazi wao mapema
- kabla ya kutangaziwa umma kuhusu uteuzi.
- e. Inatarajiwa kuwa Kamati ya Tuzo itatangaza uteuzi wake muda mfupi baadaye, pakiwepo
- Mwenyekiti na/ama wale wanachama wa Kamati ya Tuzo wanaoweza kuhudhuria kikao
- cha waandishi wa habari.
- Afisi Kuu pamoja na Halmashauri na Kamati ya Tuzo watatayarisha tanbihi ya kielelezo itakayopewa Mshindi katika hafla rasmi ya Tuzo.
- Tuzo linakusudiwa kuwapa hamasa viongozi wanaojitolea katika enzi zao za uongozi kupambana na majukumu ya maendeleo ya nchi zao, kuimarisha hali za maisha za raia wake na kuweka mikakati ya kuweka misingi ya maendeleo ya kujitegemeza. Inatarajiwa kuwa Tuzo hili litaimarisha mijadala katika jamii kuhusu ni vigezo vipi vitakavyotumiwa kuangalia rekodi za serikali. Katika kumteua Mshindi wa Mo Ibrahim, Kamati ya Tuzo itadurusu vigezo vifuatavyo-
- Tuzo litatolewa kwa sababu ya ubora wa nchi zao kiutendaji kazi muda ule walipokuwa mamlakani, ikilinganishwa na mataifa mengine ya Afrika kusini mwa Sahara.
- Maendeleo ya Kitaifa sharti yaonekane katika maeneo haya ya kiutawala.
- Maendeleo ya kiuchumi yanayojitegemeza
- Maendeleo ya kijamii: Afya na Elimu
- Uwazi, ikiwemo vita dhidi ya ufisadi, na kuzipa nguvu mashirika ya kijamii
- Demokrasia na haki za kibinadamu
- Utawala unaozingatia sheria na usalama.
- Kuhakiki utendaji kazi sharti kuwe wa haki, kukizingatiwa Kigezo cha Ibrahim na uchanganuzi unaotambulika.
- Maelezo na yaliyojadiliwa ya Kamati ya Tuzo ni ya siri. Hakuna mwanachama wa
- Kamati ya Tuzo atakayefichua chochote kilichojadiliwa , ama hatima ya washiriki wengine, wakati wowote ule. Inatarajiwa kuwa kumbukumbu za wakfu itahifadhi vifaa kama vile karatasi za kimsingi na data na kufungiwa kwa muda wa miaka 25.
- Hakuna kwa hali zozote zile, ambapo Kamati ya Tuzo, Afisi Kuu, ama Halmashauri ya Wakfu itakutana na washiriki kujadili uwezo wao wa kushiriki. Wengine katika hali zao za kikazi huenda wakakumbana na washiriki, na kuonana huko ana kwa ana na washiriki kunaweza kusaidia Kamati ya Tuzo katika uteuzi wao, lakini bila kujadili Tuzo la Ibrahim ama yanayoambatana nalo.
- Wakfu unatilia maanani uwazi katika masiala ya uongozi na hivyo basi, majina ya wanachama wa Kamati ya Tuzo, njia ya uteuzi, Kigezo cha Ibrahim, na sababu za kimsingi za kumchagua Mshindi yatapatikana.
Fungua Masharti ya Majukumu
