Dr Mo Ibrahim

Dkt. Mo Ibrahim ni mtaalamu wa kimataifa katika mawasiliano ya rununu ambaye pia ni msomi na mfanyibiashara [mfanyabiashara] mahiri.

Mzaliwa wa Sudan, Dkt. Ibrahim ndiye mwanzilishi wa kampuni ya Kimataifa ya Celtel, mojawapo ya makampuni yaliyotia for a [ yaliyotia fora] katika Afrika.

Mnamo mwaka wa 1998, Dkt. Ibrahim alianzisha MSI Cellular Investments, ambayo hapo baadaye ilibadilishwa na kuitwa Celtel International. Kampuni hii kwa sasa inapatikana katika mataifa 15 ya Afrika, chini ya leseni ambayo inawahudumia zaidi ya theluthi moja ya idadi yote ya watu katika Afrika. Kampuni hii imeweka rasilmali ya zaidi ya dola za kimarekani [Kimarekani] milioni 750 katika Afrika, ikisaidia kuleta faida za mawasiliano ya rununu kwa mamilioni ya watu kote katika bara.

Mwaka wa 2005, kampuni ya Kimataifa ya Celtel iliuzwa kwa MTC Kuwait kwa dola za kimarekani bilioni 3.4, na kuifanya kuwa mojawapo ya biashara iliyotia fora katika Afrika.

Dkt. Mo Ibrahim ana shahada ya Bsc katika Uhandisi wa Elektroniksi kutoka Chuo Kikuu cha Alexandria, Misri, Shahada ya uzamili ya Msc katika Elektroniksi na uhandisi wa Elektroniksi kutoka Chuo Kikuu cha Bradford, na Shahada ya uzamifu, yaani PhD katika Mawasiliano ya Rununu kutoka Chuo Kikuu cha Birmingham. Ni mwanachama wa Halmashauri ya kutoa Ushauri katika eneo la Afrika katika Shule ya Biashara ya London.

Juu

Lalla Ben Barka

Lalla Ben Barka yupo katika mstari wa mbele kwenye masiala yanayohusiana na utendaji na ukarabati wa sera za kielimu kote katika Afrika.

Mtetezi wa elimu kama nyenzo za kuifanya Afrika kukua na maendeleo ya muda mrefu kiuchumi, ujuzi wa Bi. Ben Barka unajikita katika kuimarisha utoaji, kuimarisha miundo misingi ya kielimu, kuweka usalama kwa uwekezaji, kuweza kufikia teknolojia na kupinga tamaduni za kijadi, hususan katika elimu ya wanawake.

Baada ya kupata shahada katika Elimu na Saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Paris X, Bi. Ben Barka alifanya kazi kwa muda nchini Ufaransa kama Mwanasaikolojia kabla kurejea Afrika kufundisha kule Morocco na Mauritania. Baadaye alipokea shahada ya Uzamifu yaani PhD katika Elimu katika Chuo Kikuu cha Southern California, Los Angeles.

Mzaliwa wa Mali, Bi. Ben Barka amefanya kazi kama mkuu wa kundi linalowatetea wanawake kujihimarisha ambalo ni kitengo cha Ujuaji Kusoma na Isimu ya Utendaji Kazi(DNAFLA) na Mradi wa Programme Decennal de Developpment de l Education(PRODEC).

Mnamo 1998, Bi. Ben Barka aliteuliwa kama Naibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa kushughulikia Uchumi wa Afrika(UNECA). Miaka sita baadaye, alishika hatamu za Mkurugenzi wa UNESCO katika masiala ya Elimu eneo la Afrika mnamo 2004, akitoa uongozi wa kimawaidha, kimikakati na utendaji katika miradi ainati ya kuboresha elimu kote katika mataifa chini ya Sahara. Katika kutambua juhudi zake za kuboresha elimu, Lalla Ben Barka alitunukiwa Tuzo la UNESCO [ Tuzo ya]Literary Prize mnamo 1993.

Juu

Lord Cairns

Lord Cairns amekuwa mfanyibiashara [mfanyabiashara] mahiri akiongoza baadhi ya Mabenki ya Uwekezaji yaliyotia for a [fora] nchini Uingereza.

Kama Mwanauchumi wa Maendeleo, Lord Cairns alikuwa Mwenyekiti wa Allied Zurich na kampuni ya BAT na pia Naibu wa Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wa SG Warburg. Kati ya 1992 na 2004, alikuwa Mwenyekiti wa Actis Capital LLP( ambayo zamani lilikuwa Kundi la CDC), mojawapo ya makampuni makubwa kabisa yenye uwekezaji katika sekta za kilimo, huduma za hela, makampuni na vifaa vya ujenzi katika nchi 18 za Afrika.

Pamoja na Cyril Ramaphosa, Lord Cairns alianzisha na kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Biashara ya Mataifa ya Commonwealth kwa kuitikia mwito wa Waziri Mkuu Tony Blair na Rais Mbeki wa Afrika Kusini. Shirika hili linaendelea kutoa nafasi kwa serikali na sekta za kibinafsi kufanya kazi kwa pamoja katika lengo la kuongeza baishara na uwekezaji katika Commonwealth, hususan Afrika.

Kati ya 1981 hadi 1992, Lord Cairns pia alikuwa mwenyekiti wa Huduma za Kujitolea Ugenini(VSO), shirika ambalo linakabiliwa na jukumu la kuwapeleka zaidi ya watu elfu moja wanaojitolea kutoa huduma kila mwaka katika miradi ya elimu, afya na ujenzi katika Afrika. Lord Cairns pia amehudumu kama Mwenyekiti wa Taasisi ya Maendeleo Ugenini, ambayo, chini ya uongozi wake, imepanuka maradufu na kuongeza kwa kiwango kikubwa huduma zake.

Juu

Mamphela Ramphele

Mamphela Ramphele ni mkereketwa wa haki za kijamii nyumbani na ugenini.

Akikulia Afrika ya Kusini wakati wa ubaguzi wa rangi, Dkt. Ramphele alikuwa mwanaharakati mkuu katika siasa za wanafunzi na mmoja wa waanzilishi wa Vuguvugu la Kuwahamasisha Weusi(BCM) pamoja na mwenzake Steve Biko. Mnamo 1977, Dkt. Ramphele alitiwa nguvuni na kutoruhusiwa kutoka Kaskazini mwa Transvaal kwa miaka saba. Akiendelea na kampeini yake ya kutaka weusi kupata uhuru na haki, alianzisha Mradi wa Kijamii wa Afya wa Ithuseng.

Mwaka 1986, Dkt. Ramphele alijiunga na Chuo Kikuu cha Cape Town kama Mtafiti. Miaka kumi baadaye, aliteuliwa kama Naibu wa Chansela, hivyo akawa mwanamke wa kwanza mweusi kupata cheo hicho katika Chuo Kikuu kilichoko Afrika Kusini.

Dkt. Ramphele alijiuzulu kutoka wadhifa huo mwaka wa 2000 na kujiunga na Benki ya Dunia kama Mkurugenzi Mkuu, akiwa ni mwafrika wa kwanza na akiwa mwanamke wa pili kuushikilia wadhifa huo. Majukumu yake yalikuwa ni pamoja na kusimamia huduma za benki katika sekta za elimu, afya, lishe, idadi ya watu na usalama wa kijamii.

Mwaka wa 2004, Dkt. Mamphela Ramphele aliteuliwa kama Mwenyekiti Msaidizi wa Umoja wa Mataifa wa Uhamiaji, shirika ambalo linachunguza nafasi na matatizo ya kitaifa na kimataifa yanayotokana na uhamiaji barani Afrika na kwingine Ulimwenguni. Pia yeye alikuwa mwenyekiti wa Halmashauri ya Wadhamini wa Independent Deveopment Trust(IDT), ambalo ndilo shirika lisilo la kiserikali lililo kubwa zaidi Afrika ya Kusini katika kuwapa watu nguvu za kujisimamia.

Juu

Mary Robinson

Mary Robinson amekuwa mkereketwa wa mstari wa mbele katika haki za binadamu maishani mwake mwote.

Akichaguliwa kama Rais wa kike wa kwanza wa Ireland mnamo 1990, Bi. Robinson anatambuliwa kwingi kama aliyeanzisha uhusiano maalum kati ya Ireland na mataifa ya ulimwengu yanayoendelea. Mnamo 1992, Bi. Robinson alikuwa ndiye kiongozi wa nchi ya kwanza kuitembelea Somalia ilipokumbwa na janga la njaa, na pia alikuwa wa kwanza kuitembelea Rwanda baada ya mauaji ya maelfu ya watu.

Mwaka wa 1997, kwa kutambua kujitolea kwake kuhusu haki na usawa, Katibu Mkuu wa UM Kofi Annan alimteua Bi. Robinson Kamishena Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu.

Tangu atoke UM mnamo 2002, Bi. Robinson ameendelea kuyatetea masiala ya mataifa yanayoendelea kupitia Utambuzi wa Haki, mradi wa kimaadili wa Kiulimwengu unaopigania haki na usawa katika biashara, na kuimarisha harakati za kupambana na virusi vya HIV na Ukimwi na kuweka mikakati thabiti za sera za uhamiaji za binadamu.

Mary Robinson ametambuliwa ulimwenguni kote kutokana na juhudi hizi zake. Mnamo 2004, alifanywa balozi wa shirika la Kimataifa la Amnesty kama ‘Balozi wa Ufahamu wa Nafsini’. Yeye pia ni Rais wa Heshima wa shirika la kimataifa la Oxfam.

Juu

Salim Ahmed Salim

Salim Ahmed Salim ni mmoja wa viongozi stadi waasisi katika mambo ya kiutawala barani Afrika.

Alisomea vyuo vikuu vya Delhi na Columbia. Bw. Salim alianza kazi kama mwanasiasa katika udiplomasia wa kimataifa, akiwa balozi huko Misri(1964-1965), balozi kule India(1965-1968), balozi katika taifa la Uchina(1969) na mwakilishi wa kudumu wa UM kule New York(1970).

Akiwa kama mmoja wa wale waliokuwa katika mstari wa mbele kupiga vita dhidi ya ubaguzi wa rangi, Bw. Salim amehudumu kama Mwenyekiti wa Kamati ya Tume ya Umoja wa Mataifa iliyoshughulikia uwekaji wa vikwazo dhidi ya Rhodesia, Rais wa Kongamano la Kimataifa la Vikwazo dhidi ya Afrika Kusini na Rais wa Kongamano la Kimataifa la Paris kuhusu Ubaguzi wa Rangi. Akihudumu kama Mwenyekiti wa Umoja wa Mataifa wa Kamati Maalum ya Kujinasua kutokana na Ukoloni, alisaidia katika kuleta enzi mpya ya kupata uhuru katika bara.

Aliteuliwa kama Rais wa Umoja wa Mataifa wa Kamati ya Kiusalama mnamo 1976 na akahudumu kama Rais wa kikao cha Thelathini na Nne ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mnamo Septemba 1979.

Akitoka UM mnamo 1980, Salim Ahmed Salim alirudi Tanzania ambapo alijihusisha na siasa za nyumbani, akishikilia nyadhifa za juu serikalini kama waziri ikiwemo Waziri Mkuu (1984-85). Baadaye aliteuliwa kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika(OAU), na kuuelekeza hadi kuwa Muungano wa Afrika (AU).

Juu

Nicholas Ulanov

Nicholas Ulanov ni mtaalamu wa kutoa ushauri wa mikakati na usimamizi wa sekta zisizokuwa za kupata faida.[zisizo za kupata faida]

Shirika la Ulanov, ambalo lilianzishwa na Bw. Ulanov miongo miwili iliyopita, linahudumia taasisi muhimu zinazowafaidi umma kote ulimwenguni. Limeshiriki na kuchangia kuleta utendaji kazi bora katika elimu, misingi, sera za umma, sanaa, makavazi, na pia nyanja nyingine zisizo kuwa za kupata faida[zisizo za kupata faida] katika nchi mbalimbali, hii ikiwa ni katika bara sita.

Kabla ya kulianzisha shirika hili lake, Bw. Ulanov alikuwa mshauri wa vyombo vya habari na mawasiliano katika McKinsey & Company, ambapo aliegemea upande wa vyombo vya zamani na vipya vya habari kati ya mpaka mmoja na mwingine katika kila lugha kuu, na kujiingiza katika tarakilishi na teknolojia ya juu ya utafiti na maendeleo.

Kama mshauri miaka ya tisini, Bw. Ulanov alikuwa ndiye uti wa mgongo wa Kampeini ya Oxford, ya Chuo Kikuu cha Oxford, kampeini ya hela ya kwanza nje ya Marekani iliyokusanya zaidi ya pauni milioni 300 na kujaza nafasi za wasomi 200. Kama sehemu ya kazi yake na Oxford, alihudumia kwa miaka miwili kama mkurugenzi mkuu wa afisi zake za Kaskazini mwa Marekani kule New York na Toronto.

Nicholas Ulanov ni mwasisi wa Royal Institution World Science Assembly, akileta pamoja sayansi na siasa katika jamii katika masiala kama hatari za homa ya kuku na magonjwa mengine. Alikuwa mwakilishi wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali huko Umoja wa Mataifa wa Taasisi ya Pate, likifanya kazi ya mwanzilishi wa Umoja wa Mataifa wa Elimu na Hazina ya Watoto(UNICEF) Maurice Pate, na pia kama msomi wa ufadhili wa Rhodes katika chuo kikuu cha Oxford, angali ni mshiriki thabiti katika vitendo vya vyuo vikuu na taasisi za juu za usomi kote ulimwenguni.

Juu