Geneva, Switzerland - Jumatatu Aprili 2 2007

Kofi Annan ateuliwa kama mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Tuzo la Mo Ibrahim

Wakfu wa Mo Ibrahim yatangaza kamati ya kumteua mshindi wa tuzo kubwa ulimwenguni.

Kofi Annan, aliyekuwa Katibu Mkuu wa UM, atasaidiwa na watu watano waadilifu kwenye Kamati ya Tuzo ambayo itamteua mshindi wa tuzo kubwa ulimwenguni: Tuzo la Mo Ibrahim la Kufaulu kwa Uongozi wa Kiafrika. Tangazo hili linatolewa baada ya Kamati ya Tuzo kukutana kwa mara ya kwanza wikiendi hii kule Geneva, Switzerland.

Tuzo lina thamani ya dola za kimarekani milioni tano kwa kipindi cha miaka 10 na dola za kimarekani elfu 200,000 baadaye kila mwaka wakati wote wa uhai wake. Tuzo linapaswa kutunukiwa kwa Kiongozi mstaafu wa taifa ama serikali ya Afrika chini ya Sahara ambao wameacha uongozi miaka mitatu iliyopita na kuonyesha uongozi wa kipekee.

Bw. Annan anasaidiwa katika Kamati na wafuatao:

  • Martti Ahtisaari, aliyekuwa Mwakilishi Maalum wa UM huko Namibia na Rais mstaafu wa Finland
  • Aïcha Bah Diallo, aliyekuwa Waziri wa Elimu Guinea na Mshauri Maalum kwa Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO
  • Ngozi Okonjo-Iweala, aliyekuwa Waziri wa Fedha na pia aliyekuwa Waziri wa Mashauri ya Nje wa Nigeria
  • Mary Robinson, aliyekuwa Rais wa Ireland na Kamishena wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu(na mwanachama wa Halmashauri ya Wakfu)
  • Salim Ahmed Salim, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika(na mwanachana wa Halmashauri ya Wakfu)

Kamati hii itamtathmini kila kiongozi wa Afrika chini ya Shara ambaye tayari ameacha mamlaka miaka mitatu iliyopita kwa mujibu wa uongozi wao. Wakfu utatangaza mshindi wa kwanza wa Tuzo mnamo Oktoba 22 2007.

Kamati itategemea pia utafiti unaotokana na Kigezo cha Ibrahim cha Uongozi Kiafrika, na chimbuko jingine, na kutathmini ubora wa uongozi katika maendeleo ya maeneo ya kiuchumi na kijamii, amani na usalama, haki za kibinadamu, demokrasia na utawala wa kisheria. Tuzo linanuia kuwapa motisha viongozi ambao wamejitolea muda ule walioko afisini to kuanzisha maendeleo katika nchi zao, kuimarisha hali za watu wao na kuweka msingi imara ya maendeleo anayojitegemeza.

 

Akiongea huko Geneva wakati wa kutangazwa kwa Kamati, Bw. Anna asema:

"Jukumu lililoko mbele yetu-la kumteua kiongozi bora katika Uongozi wa Kiafrika-ni kubwa. Ingawa mataifa yaliyositawi yana mchango muhimu katika kuleta hali njema ya kuleta maendeleo, ni jukumu la Afrika kuongeza na kushika hatamu za kumiliki maendeleo ya Afrika. Uongozi thabiti na utawala na muhimu katika kupata suluhisho la matatizo yanayoikabili Afrika. Tunatumai kuwa Tuzo la Mo Ibrahim litakuwa changamoto kwa Uongozi wa Kiafrika na kuwapa hamasa viongozi vijana kukabiliana na majukumu haya."

 

Dkt. Mo Ibrahim, mwasisi wa Wakfu wa Mo Ibrahim, anasema:

"Nina furaha tele kuwa na watu wote hawa hapa leo. Wakfu utafaidika na busara na tajriba ya Bw. Annan, Bw. Ahtisaari, Bi. Okonjo-Iweala, Bi. Bah Diallo, Bi. Robinson na Bw. Salim. Tuzo hili na Kigezo cha Ibrahim, tunatumai kuchangia kwa njia ya kipekee katika kutathmini uongozi na kutambua uongozi katika Afrika."

 

MWISHO

 

ANWANI

Robert Watkinson
+ 44 (0)20 7421 6143
robert.watkinson@portlandpr.co.uk


Picha za mkutano wa uzinduzi za Kamati ya Tuzo zitapatikana kupitia AFP kuanzia 09.00 GMT, Jumatatu tarehe 2 Aprili.

 

Matini kwa wahariri:

  1. Wakfu wa Mo Ibrahim ni ndoto ya Dkt. Mo Ibrahim, mwanzilishi wa kampuni ya mawasiliano ya Afrika ya Celtel International na mmoja wa wafanyibiashara aliyetia fora barani Afrika, na ambao umeanzishwa ili kufanikisha uongozi thabiti katika Afrika. Ni shirika lisilo la kupata faida na Wakfu wenyewe unasimamiwa na halmashauri ya wadhamini ulio na wanachama wengine wakiwemo Dkt. Mo Ibrahim (Mwanzilishi, Kampuni ya Kimataifa ya Celtel); Lalla Ben Barka (Mkurugenzi wa Kimaeneo UNESCO, Masiala ya Elimu); Lord Cairns(Mwenyekiti, Wakfu wa Msaada wa Ufadhili); Dkt. Mamphela Ramphele(Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Dunia); Mary Robinson (Aliyekuwa Rais wa Ireland na aliyekuwa Kamishena Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu); Salim Ahmed Salim (Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika) na Nicholas Ulanov(Mkurugenzi Mkuu,Ushirika wa Ulanov).
  2. Kigezo cha Ibrahim cha Uongozi wa Kiafrika ni kipya na kipevu ya kuyaweka katika daraja ya mataifa kusini mwa Sahara kwa misingi ya ubora wa uongozi. Kimetayarishwa chini ya uelekezi wa Profesa Robert Rotberg, wa shule ya Kennedy ya Serikali katika Chuo Kikuu cha Harvard. Kigezo cha Ibrahim kinanuia kuhamamisha mjadala sio tu katika Afrika bali kote ulimwenguni kuhusu ni vigezo vipi vitakavyotumiwa katika kuzitathmini serikali.
  3. Tuzo la Mo Ibrahim la Kufaulu kwa Uongozi la Kiafrika linawatambua viongozi wa Afrika ambao wameonyesha ukakamavu katika uongozi wa kisiasa. Tuzo hili na ambalo ndilo kubwa duniani linadhihirisha umuhimu wa kuwalea viongozi bora barani Afrika. Tuzo litahusisha dola za kimarekani milioni 5 katika kipindi cha miaka 10 na dola za kimarekani elfu 200,000 baadaye kila mwaka wakati wote wa uhai wake. Isitoshe, zipo dola za kimarekani 200,000 kila mwaka kwa miradi mizuri itakayobainiwa na mshindi na zinaweza kutolewa na wakfu huo kama utakavyoamua katika kipindi cha miaka 10 ya mwanzo. Tuzo la Mo Ibrahim ndilo kubwa kote ulimwenguni linalotolewa kila mwaka.

www.moibrahimfoundation.org

Juu

Fungua taarifa ya habari iliyoko hapo juu
pdf

 

Alhamisi 26 Oktoba 2006-kutolewa mara moja

Wakfu mpya kutangaza tuzo lililo kubwa Ulimwenguni

Nelson Mandela na viongozi wa dunia waupongeza mradi ambao “utaimarisha ufufuzi wa kisiasa na kiuchumi katika Afrika”

Viongozi wa dunia, akiwemo Nelson Mandela, Kofi Annan, Bill Clinton na Tony Blair leo wanaunga mkono mradi mpya kabambe unaozinduliwa kuimarisha na kutambua uongozi thabiti katika Afrika.

Wakfu wa Mo Ibrahim, ulioanzishwa na Dkt. Mo Ibrahim, mwanzilishi wa kampuni ya Kimataifa ya Celtel, unazinduliwa leo asubuhi jijini London. Akiandamana na wanachama wa Halmashauri wakiwemo Mary Robinson na Salim Ahmed Salim, Dkt. Mo Ibrahim atatangaza:

  • Kigezo changamano kuupima na kuutathmini uongozi thabiti katika Afrika kwa msingi wa taifa moja baada ya jingine na kilichotayarishwa chini ya uelekezi wa Profesa Robert Rotberg, wa shule ya Kennedy ya Serikali katika Chuo Kikuu cha Harvard.
  • Yaliyomo kuhusu Tuzo kubwa duniani la Tuzo la Mo Ibrahim la Kufaulu kwa Uongozi wa Kiafrika, litakalotunukiwa viongozi waliostaafu wan chi ama serikali za Afrika na ambao wamedhihira uongozi thabiti. Tuzo litahusisha dola za kimarekani milioni 5 katika kipindi cha miaka 10 na dola za kimarekani elfu 200,000 baadaye kila mwaka wakati wote wa uhai wake. Isitoshe, zipo dola za kimarekani 200,000 kila mwaka kwa miradi mizuri itakayobainiwa na kiongozi.

Kwenye hafla ya uzinduzi wa Wakfu huo, Dkt. Mo Ibrahim atasema: “Hamna, kamwe hamna kilichoko muhimu zaidi kwa Afrika kuliko uongozi thabiti. Leo, nauzindua wakfu ambao unanuia kubadilisha kwa upeo mkubwa hali zinazowakabili viongozi wa Afrika, na kwa mintarafu hii, kupiga msasa upya mjadala wa uongozi.”

Nelson Mandela asema: “Mo Ibrahim ana ndoto ya kuimarisha na kutambua utawala thabiti ambao utaimarisha ufufuzi wa kisiasa na kiuchumi katika Afrika... Huu ni mradi wa Kiafrika unaosherehekea ushindi wa uongozi mpya wa Kiafrika. Unatoa mfano ambao maeneo mengine ya ulimwenguni yanaweza kuiga. Tunatoa mwito kwa viongozi wote kote duniani-serikalini, mashirika ya umma na biashara-kuunga mkono malengo yake na ndoto yake.”

Kofi Annan, Katibu Mkuu,Umoja wa Mataifa asema: “Shukran kwa ndoto ya Mo kwa sababu wakfu utachangia katika vuguvugu la kupatikana kwa uongozi wa haki na wenye uono barani Afrika. Inaweza kuwatia hamasa kizazi kijacho kuiga hali za juu za utumishi kwa umma, na inaweza ikatoa zile cheche za kipekee za ubunishi ambazo zinazalisha sekta za kibinafsi na za umma kwa pamoja.”

Bill Clinton, aliyekuwa Rais wa Marekani asema: “Mo Ibrahim ameanzisha Wakfu wa Afrika kuisaidia Afrika kusonga mbele... namshukuru Mo Ibrahim kwa uongozi anaothibitisha, tuzo ambalo sote tutaweza kulitumia-enzi za usoni bora kwa watoto wetu.”

Tony Blair MP, Waziri Mkuu wa Uingereza, asema: “Ni jukumu la viongozi wa Afrika kuisukuma mbele sera na mipango ya kupunguza umaskini... Wakfu unanuia kutuza na kuhimiza uongozi wa kipekee-lengo ambalo naliunga mkono kwa dhati. Nautakia wakfu kila la heri katika jukumu hili muhimu.”

Paul Wolfowitz, Rais wa Benki ya Dunia, asema: “Ningependa kumshukuru Dkt. Ibrahim na Wakfu wa Mo Ibrahim kwa ndoto yao na usaidizi ambao wanatoa kwa viongozi hao wa Afrika ambao wanatambua kuwa kuhifadhi viwango vya juu vya uongozi ndiko njia bora na yenye matokeo mema kwa maisha ya raia wa Afrika.”

Alpha Oumar Konaré, Mwenyekiti, Muungano wa Afrika, asema: “Naipongeza ndoto hii ambayo ni mradi wa kusifika kuutambua uongozi wenye busara na wenye malengo. Utasaidia kuleta uongozi bora, utawala wa sheria, na kuingizwa kwa demokrasia na vipengele vyake vyote.”

Profesa Amartya Sen, Mshindi wa Tuzo la Nobel katika Uchumi, asema: “Mradi wa Tuzo la Mo Ibrahim ni hatua muhimu katika kuendeleza hali za juu za uongozi wa kisiasa ambayo inaweza kuwa muhimu katika kuimarisha haliza wakazi wa Afrika na nguvu za mashirika ya umma.”

 

Matini kwa wahariri:

Uzinduzi utafanyika katika Atrium, 4 Millbank, Westminster, SW1P 3JA kuanzia saa 2.45 asubuhi mnamo Alhamisi Oktoba 26. Mashirika yote ya habari yanaalikwa.

Mnamo Ijumaa 27 Oktoba kwa ushirikiano na Kituo cha Masomo ya Afrika (CAS) katika Chuo Kikuu cha London, Wakfu utakuwa na kikao cha mjadala chenye kichwa ‘Uwekaji Kigezo cha Uongozi Thabiti katika Afrika’. Wakfu baadaye utazitembelea Nairobi na Johannesburg.

Kwa mengi zaidi kuhusu Wakfu wa Mo Ibrahim, Tuzo la Mo Ibrahim la Kufaulu kwa Uongozi wa Kiafrika na Kigezo cha Ibrahim cha Uongozi katika Afrika, tafadhali izuru tovuti ya www.moibrahimfoundation.org

 

ANWANI

Toby Orr
Simu + 44 (0)207 404 5344
Rununu: + 44 (0)7736 175311
toby.orr@portlandpr.co.uk

Robert Watkinson
Simu + 44 (0)207 404 5344
Rununu: + 44 (0)7984 433486
robert.watkinson@portlandpr.co.uk

 

  1. Wakfu wa Mo Ibrahim ni ndoto ya Dkt. Mo Ibrahim, mwanzilishi wa kampuni ya mawasiliano ya Afrika ya Celtel International na mmoja wa wafanyibiashara aliyetia fora barani Afrika, na ambao umeanzishwa ili kufanikisha uongozi thabiti katika Afrika. Ni shirika lisilo la kupata faida na Wakfu wenyewe unasimamiwa na halmashauri ya wadhamini ulio na wanachama wengine wakiwemo Dkt. Mo Ibrahim (Mwanzilishi, Kampuni ya Kimataifa ya Celtel); Salim Ahmed Salim (Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika); Mary Robinson (Aliyekuwa Rais wa Ireland na aliyekuwa Kamishena Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu); Dkt. Mamphela Ramphele(Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Dunia); Lord Cairns(Mwenyekiti, Wakfu wa Msaada wa Ufadhili); Nicholas Ulanov(Mkurugenzi Mkuu,Ushirika wa Ulanov) na Bi.Lalla Ben Barka (Mkurugenzi wa Kimaeneo UNESCO, Masiala ya Elimu).
  2. Kigezo cha Ibrahim cha Uongozi wa Kiafrika ni kipya na kipevu ya kuyaweka katika daraja ya mataifa kusini mwa Sahara kwa misingi ya ubora wa uongozi. Kimetayarishwa chini ya uelekezi wa Profesa Robert Rotberg, wa shule ya Kennedy ya Serikali katika Chuo Kikuu cha Harvard. Kigezo cha Ibrahim kinanuia kuhamamisha mjadala sio tu katika Afrika bali kote duniani kuhusu ni vigezo vipi vitakavyotumiwa katika kuzitathmini serikali.
  3. Tuzo la Mo Ibrahim la Kufaulu kwa Uongozi la Kiafrika linawatambua viongozi wa Afrika ambao wameonyesha ukakamavu katika uongozi wa kisiasa. Tuzo hili na ambalo ndilo kubwa duniani linadhihirisha umuhimu wa kuwalea viongozi bora barani Afrika.

Juu