This movie requires Flash Player 8. Get Flash
Kizazi kipya cha viongozi wa Afrika wanakabiliwa na jukumu moja kubwa: Kuwatoa mamilioni ya watu kutoka umaskini. Hili haliwezi kutatuliwa bila kuwepo na jamii iliyoimarika kidemokrasia; iliyo na sheria zinazofanya kazi;inayotoa huduma na vifaa vya afya na elimu;mashirika ya kijamii yenye nguvu; na vigezo vinavyochangia katika ukuwaji wa kiuchumi. Kwa maneno mengine, haya yote hayawezi kupatikana bila uongozi thabiti.
Wakfu wa Mo Ibrahim ni mradi wa Kiafrika ambao imeundwa ili:
- Kutoa changamoto la mjadala wa uongozi thabiti katika Afrika chini ya Sahara na duniani.
- Ili kuwapa wananchi vigezo mahsusi vya kupima na kuzilazimisha serikali zao kujiwajibika.
- Kutambua kufaulu kwa Uongozi wa kiafrika na kutoa njia mwafaka ya namna viongozi wa Kiafrika wanaweza kuwacha wasifu na hiba nzuri kwa bara hii pindi watokapo afisini.

