This movie requires the Macromedia Flash Player 8.
Get Flash

Nelson Mandela
Aliyekuwa Rais wa Afrika ya Kusini

“Mo Ibrahim ana ndoto ya kuimarisha na kutambua utawala thabiti[uongozi bora] ambao utaimarisha ufufuzi wa kisiasa na kiuchumi katika Afrika. Ameanzisha wakfu wa Mo Ibrahim kuendeleza uongozi thabiti[utawala bora], kuzua mjadala wa kiumma na kuwafanya viongozi wa bara kuweka vigezo kuhusu swala hili.

Mahsusi, Wakfu utatoa tuzo maalum kuutambua uongozi thabiti [utawala bora] kutoka kwa viongozi wa Kiafrika ambao wameshatoka mamlakani na kuacha kipindi cha hali bora wakiwa mamlakani. Ni vema kabisa tuzo hili [hii] ndilo[ndiyo] litakalokuwa [itakayokuwa]kubwa zaidi duniani. Hakuna kilicho muhimu zaidi. Tuzo litawatambua [itawatambua] viongozi wa Afrika kwa matendo yao na kutoa nafasi ya kushirikiana na mashirika ya umma na kuimarisha matendo yao mema.

Huu ni mradi wa Kiafrika unaosherehekea ushindi wa uongozi mpya wa Kiafrika. Unatoa mfano ambao maeneo mengine ya ulimwenguni yanaweza kuiga. Tunautakia wakfu mpya kila la heri na kutoa mwito kwa viongozi wote kote ulimwenguni-serikalini, mashirika ya umma na biashara-kuunga mkono malengo yake na ndoto yake. Kwa vile wakfu unanuia kutoa tuzo kubwa kuzidi yote: kusaidia katika kuhakikisha kuwa bara letu tajiri litakuwa lenye maendeleo-kwa watu wake wote.”

Juu

This movie requires the Macromedia Flash Player 8.
Get Flash

Kofi Annan
Aliyekuwa Katibu Mkuu,Umoja wa Mataifa

“Uongozi thabiti [Utawala bora] na demokrasia ni muhimu katika maendeleo ya Afrika. Bila hayo, itakuwa vigumu ama isiwezekane kwa nchi yoyote ya Afrika kufikia malengo yake ya milenia kufikia mwaka wa 2015.

Na ndiyo sababu lengo la Wakfu wa Mo Ibrahim ni muhimu. Shukran [shukrani] kwa ndoto ya Mo kwa sababu wakfu utachangia katika vuguvugu la kupatikana kwa uongozi wa haki na wenye uono barani Afrika. Inaweza kuwatia hamasa kizazi kijacho kuiga hali za juu za utumishi kwa umma, na inaweza ikatoa zile cheche za kipekee za ubunishi ambazo zinazalisha sekta za kibinafsi na za umma kwa pamoja.

Namshukuru Mo na wale wote wanaohusika na kuanzishwa kwa tuzo hili [hii] kubwa kama njia ya kutoa motisha. Linadhihirisha [Inadhihirisha] hekima ya Mo kama Mwafrika na Mo kama mfanyibiashara[mfanyabiashara] na mwekezaji. Naomba mradi wako huu kuwapa motisha na kusherehekea uongozi [utawala]bora wa Afrika na kuwahami viongozi wa usoni na hekima na tajriba ambayo watahitaji.”

Juu

This movie requires the Macromedia Flash Player 8.
Get Flash

Rais Bill Clinton
Aliyekuwa Rais wa Marekani

“Uongozi [Utawala] ni muhimu kila mahali hususan Afrika. Majukumu yanayowakabili viongozi wa Afrika ni nyeti, na maisha na hali za maisha ya mamilioni ya watu itategemea uongozi thabiti [utawala bora] wa viongozi hao.

Kwa mintarafu hii, hatuna budi kuwatambua na kuwatuza viongozi waliofaulu ambao wameweza kutoa huduma zinazoonekana kwa wananchi wao.

Wakfu wa Mo Ibrahim umeanzisha Wakfu wa Afrika kuisaidia Afrika kusonga mbele, na huo ni mfano mzuri wa Afrika kujisaidia yenyewe na kiolezo muhimu cha kusonga mbele na kuleta kukua kwa ufanisi na amani Afrika.

Ni mradi wa kutambulikana haswa kutokana na yule ambaye ni mdhamini wake. Nautakia Wakfu heri njema katika kazi yake na kumshukuru Mo Ibrahim kwa uongozi anaothibitisha, uzo ambalo sote tutaweza kulitumia-enzi za usoni bora kwa watoto wetu.”

Juu

This movie requires the Macromedia Flash Player 8.
Get Flash

José Barroso
Rais, Tume ya Ulaya

“Maendeleo ya kujitegemea yanahitaji mataifa kuwa ya kihalali machoni mwa wananchi wake na kutoa huduma kuu za kutolewa na taifa. Hii ndiyo sababu Muungano wa Ulaya umeanzisha mradi wa uongozi kwa kuongeza ufadhili zaidi wa kihela-takriban Euro bilioni 3-kwa yale mataifa ya Afrika ambayo yameitikia mwito wetu wa kuwa na mikakati mizuri ya kuleta mabadiliko katika uongozi imara. Kigezo cha African Peer Review, mfumo wa mataifa ya Afrika kujitathmini yenyewe kwa yenyewe kitakuwa muhimu kwetu. Mataifa 26 ya Afrika tayari yamejiandikisha kwa mradi huu.

Ni kwa sababu zizi hizi ndipo nazikaribisha juhudi za Wakfu wa Mo Ibrahim katika kuleta uongozi thabiti[utawala bora] na kuimarisha Uongozi wa Kiafrika. Nataka kukuhakikishia kuwa Muungano wa Tume ya Ulaya imejitolea ipasavyo, na mimi nimejitolea kibinafsi kwa malengo hayo na katika thamani ya Muungano wa Ulaya na ushirikiano wa Afrika.

Ni kupitia kwa juhudi za kiulimwengu tu ndipo mwongo huu kama eneo la chemchemi ya maji katika historia ya bara zetu[mabara yetu]. Katika kufanya hivi, hatuwezi kujitia hamnazo bali kutenda; na hili ndilo tunalolifanya.”

Juu

Mhe. Tony Blair MP
Waziri Mkuu wa Uingereza na Ireland ya Kaskazini

“Afrika imeanza kupiga hatua katika vita vya muda mrefu dhidi ya umaskini. Uingereza na mataifa mengine tajiri yana mchango wake. Katika mkutano wa Gleneagles mnamo 2005, kwa kuungwa mkono kwa dhati, matifa [mataifa] manane yenye utajiri mkubwa duniani (G8) zilikubali [yalikubali]kutoa dola za kimarekani [Kimarekani]bilioni 50 zaidi kila mwaka kama msaada kufikia 2010 na kuongeza maradufu msaada kwa Afrika. Na sasa tunafanya kazi kuhakikisha kuwa ahadi hizi zinatekelezwa.

Lakini hiyo ni sehemu tu ya picha. Hakika Afrika inahitajika kuchukua mstari wa mbele katika kuyaongoza maendeleo ya Afrika. Ni jukumu la viongozi wa Afrika kuisukuma mbele sera na mipango ya kupunguza umaskini. Ni viongozi wa Afrika wanaopaswa kupigana na ufisadi. Ni viongozi wa Afrika wanaopaswa kukomesha uongozi mbaya[utawala mbaya]. Wakfu wako mpya unanuia kutuza na kuhimiza uongozi wa kipekee-lengo ambalo naliunga mkono kwa dhati. Nautakia wakfu kila la heri katika jukumu hili muhimu.”

Juu

Profesa Amartya Sen
Profesa katika Chuo Kikuu cha Lamont, na Profesa wa Uchumi na Falsafa, Chuo Kikuu cha Harvard

“Mradi wa Tuzo la [Tuzo ya] Mo Ibrahim ni hatua muhimu katika kuendeleza hali za juu za uongozi wa kisiasa ambayo[ambao] inaweza [unaweza]kuwa muhimu katika kuimarisha haliza [hali za] wakazi wa Afrika na nguvu za mashirika ya umma. Ni matumaini yangu kuwa utachangia sio tu katika uongozi thabiti[utawala bora] kwa wale viongozi walioko afisini[ofisini], lakini pia kutoa himizo kwa viongozi wa usoni wa Afrika.

Natumai pia kuwa utazalisha mijadala ya kujenga kote katika Afrika kuhusu masiala ya uongozi na mahsusi namna inavyoweza[unavyoweza] kuchangia katika kuleta maisha bora na usalama kwa wote. Tuna sababu ya kuwa na matumaini makubwa kutokana na ndoto hii, ambayo inaweza ikaisaidia Afrika kuweza kufikia uwezo wake wa kupata faida kutokana na hali ya dunia kuwa mahala pamoja[moja].”

Juu

Alpha Oumar Konaré
Mwenyekiti, Muungano wa Afrika

“Naipongeza ndoto hii ambayo ni mradi wa kusifika kuutambua uongozi wenye busara na wenye malengo.

Bara la Afrika kwa muda mrefu limejulikana kama Bara la Giza la Dunia [duniani] kwa sababu ya viongozi wetu, waliopita na wa sasa, kutoweza kukabiliana na majukumu yanayowakumba watu wetu. Mradi huu wa kutuza heshima kwa masiala ya kikatiba utaunga mkono juhudi za awali za kukuza uongozi [utawa la]kufikia upeo wa juu zaidi katika harakati za kupigana vita dhidi ya umaskini na magonjwa, na kuhakikisha maendeleo mazuri yanapatikana.

Kwa niaba ya Tume na Muungano, kwa kila namna naiunga [nauunga] mkono na kuhimiza mradi wako, kwa sababu ambavyo utasaidia kuleta uongozi [utawala] bora, utawala wa sheria, na kuingizwa kwa demokrasia na vipengele vyake vyote.”

Juu

Louis Michel
Kamishena wa Ulaya wa Msaada wa Kibinadamu na Maendeleo ya Kimataifa

“Bila ya kuwepo na hatua kabambe za uongozi, Malengo ya Milenia ya Maendeleo hayatatimizwa. Msaada wa ziada pekee yake hautatoa matokeo bila kuwepo na kule kujitolea mhanga kwa taifa lenye linatenda[linalotenda] kazi na uwezo wa taifa la kuhusisha wataalamu wake kufanya kazi. Kwa hivyo, naukaribisha lengo jipya la uongozi lililo pevu kwa wanaohusika na maendeleo.

Ni ajenda ngumu ambayo inaweza kufaulu tu iwapo itasukumwa na viongozi wa kisiasa ambao wataweka kwa pamoja ndoto, nguvu na ujasiri wa kuiona kuwa inafaulu. Ikiwa nia ya kisiasa ipo, ni muhimu kuunga mkono kisiasa na kifedha njia ya kuleta mabadiliko. Hii ndiyo sababu Tume ya Ulaya imeamua kuongeza msaada wake kuzisaidia nchi za Afrika, Caribbea na Pacific ambazo zimeonyesha mipango kabambe ya kufanya mabadiliko.

Ninaamini kuwa Mo Ibrahim na mradi huu unaotayarishwa na Wakfu wake utatoa msaada muhimu kwa juhudi hizi za kinyumbani kuhusu uongozi[utawala], kwa vile ambavyo zitaimarisha utambuzi na kuongeza uono katika masiala ya uadilifu na uongozi [utawala] wa kujitolea katika bara la Afriak[Afrika].”

Juu

Jeremy Hobbs
Mkurugenzi Mkuu, Shirika la Kimataifa la Oxfam

“Kwa niaba ya Shirika la Kimataifa la Oxfam, ningependa kuunga mkono kwa dhati kuanzishwa kwa wakfu wa Mo Ibrahim na kazi yake katika kutoa heshima katika ubora wa uongozi wa Kiafrika na kuendeleza matokeo mema na masiala nyeti ambayo yanawakumba viongozi katika bara la Afrika...

Oxfam kwa muda mrefu limeshikilia msimamo kuwa suluhisho kwa matatizo yanayoikumba Afrika limo mikononi mwa Waafrika wenyewe chini ya viongozi shupavu wa Afrika... kila jitihada ambayo inanuia kuimarisha hali za watu wa Afrika inapaswa kuungwa mkono, kwa vile ndiyo ufunguo wa mabadiliko na ufanisi. Oxfam litazidi kufanya kila liwezalo kuwasaidia watu wa Afrika na jamii husika kufikia haki zao na tunatazamia kufanya kazi na wakfu huu mpya katika siku za usoni.”

Juu

David Nussbaum
Mkurugenzi Mkuu, Shirika la Kimataifa la Transparency

“Kuhimiza uadilifu katika uongozi wa kisiasa ni muhimu kote ulimwenguni, na hususan katika Afrika. Hata hivyo, vikwamizi vya kutowezakana kwa hayo ni vingi. Mikakati ya kubuni inahitajika, na ninatumai kuwa juhudi hizi za Wakfu wa Mo Ibrahim itachangia pakubwa katika kuleta mabadiliko kwa namna ambavyo mageuzi ya kisiasa yanavyotokea katika bara. Mseto wa kuzitambua juhudi na ufanisi wa siku zilizopita, na wakati huo kuwapa motisha wale watakaotoa uongozi siku za usoni, inaweza kuwa changamoto katika kuleta uongozi thabiti[utawala bora].

Ufanisi wa juu katika tuzo hili[hii] lisilo la [isiyo ya ] kawaida halitakuwa[haitakuwa] kutoa usalama wa kifedha kwa wachache, lakini katika kuimarisha maendeleo makubwa na hali za watu. Hiyo ndiyo ndoto na lengo ambalo mradi huu unatarajia kuchangia.”

Juu